prpr

Proin na Ubelgiji kuuza Movie Online

By:
May. 1st, 2015
 Mwenyekiti wa Proin Group Tanzania ndugu Johnson Lukaza akizungumza machache na kuwashukuru watu wote waliohudhuria uzinduzi wa manunuzi ya filamu za kitanzania kupitia mtandao (online) hapo jana katika ukumbi wa ACP House jijini Brussel nchini Ubelgiji na kuudhuriwa na watu wa mataifa mbalimbali.Uzinduzi huo ulifanywa na balozi wa Tanzania Mheshimiwa Diodorus Kamala.
Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji Mheshimiwa Diodorus Kamala[l] akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wageni waalikwa kutoka mataifa mbalimbali katika uzinduzi wa uuzaji wa filamu za kitanzania ambazo sasa zitakuwa zikiuzwa online.Sherehe hizo za uzinduzi ambazo zilifanyika jijini Brussel nchini Ubelgiji na kuhudhuriwa na watu mbalimbali.
Dr.Pendo akifanya mahojiano machache na Mheshimiwa Emmanuel kuhusiana na Filamu za kitanzania ambazo zitakuwa zikiuzwa mitandaoni popote duniani.
Mwenyekiti wa Proin Group Tanzania ndugu Johnson Lukaza [r] akiwa na viongozi wa Kitanzania nchi Ubelgiji katika sherehe za uzinduzi wa manunuzi ya filamu za kitanzania onlione.
Kiongozi wa watanzania nchini Ubelgiji bwana Macha[r] akiwa na kiongozi wa watanzania jijini Antwerpen kwenye uzinduzi wa manunuzi ya filamu za kitanzania online popote duniani
Mwenyekiti wa Proin Group bwana Johnson Lukaza [l] akiwa na mmoja wa wageni waalikwa katika uzinduzi wa manunuzi ya filamu za kitanzania online jijini Brussel nchini Ubelgiji hapo jana.
Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji,Mheshimiwa Dr.Kamala akibadilishana mawazo na wageni wake mara tu baada ya uzinduzi wa manunuzi ya filamu za kitanzania online duniani kote.Balozi ni mmoja wa washiriki waliofanikisha shughuli nzima ya uzinduzi huo.
Warembo kutoka mataifa mbalimbali walikuwepo kwenye uzinduzi huo hapo jana.kwa manunuzi ya filamu zote za kitanzania sasa waweza kununua popote pale duniani kwa kutembelea website hii ya www.proinpromotions.co.tz  Pendelea vya kwenu kwa kununua vyenu,sheme Watanzania,Warundi,Wanyarwanda,Wakongo,Wazambia,Waganda,Wakenya na waafrika woote tunaomba ushirikiano wenu kwa kununua filamu zetu sasa.

Create AccountLog In Your Account