Mwanaafa Mwinzago

MWANAAFA AANZA SHULE

By:
Jan. 13th, 2015

Mshindi wa Milioni Hamsini za Shindano la Tanzania Movie Talents 2014, Ameanza shule kama alivyoahidiwa na mwenyekiti Proin group. Mwanaafa Ambaye mwaka jana alishinda kwa kuwa muigizaji bora katika ya 20 walichaguliwa kutoka Tanznaia nzima ameanza kusoma katika shule ya msingi ya Green Acres.

Mbali na Shule, Pia sinema ambayo mwaanafa amaekuwa kama muigizaji mkuu imeakamilika na inategemea kutoka mwezi wa pili mwishoni, hii ni sinema iliyoigizwa na Kumi bora ya shindano la TMT 2014. Sinema ni ya kisasa huku ikiwa imeshirikisha waigizaji wengi zaidi chipikizi pamoja na wakongwe katika Tasnia hii ya Filamu Tanzania.

Hivi karibuni Utambulisho rasmi wa sinema hii itafanyika na hivyo tusubiri mazuri kutoka kwa mwanaafa

Create AccountLog In Your Account